Ruge Mutahaba Mkurugenzi Clouds Media |
RUGE:
As a country we need to discuss issue kwa maendeleo ya nchi,
tuachane na ku-discuss ishu hizi kama personal issue.
Ni kweli kwamba tulikuwa hatutaki kulizungumzia hili na hata
sasa, ila kutokana na msukumo ladba ni vizuri kuliongelea, ila uamuzi ulikuwa
ni wetu kama tuongee au tusiongee.
Sometimes unahisi unahitaji kusikia upande wa pili, kwa
binadamu yoyote, kwa maana kuna watu ambao wanaishi mbali na hapa mjini kama
Kigoma nao wanapenda kujua juu ya swala hili kwa upande wa pili likoje.
Ila tu niseme ni tatizo la mtu binafsi halina sababu ya
kujadiliwa na kufanywa kama ni suala la kitaifa, sababu sura inayowekwa ni kama
kitu kikubwa sana, binafsi bado sijajua nini hasa tatizo la kinachojadiliwa.
Ikumbukwe kwamba Clouds ni chombo binafsi, ni chombo ambacho
kilianzishwa kwa kufata sheria zote, na sisi tulichagua namna sisi
tukavyoendesha redio yetu.
Kama biashara yoyote na sisi tunafanya biashara kutokana na
mipango yetu, na ndio maana kwa kipindi cha miaka 10 tumefanikiwa kwa kiasi
kikubwa.
Hakua anayefanya sawa duniani akakosa kulaumiwa, sisi ni
binadamu na tuna makosa ya kibinadamu kama binadamu wa kawaida.
Nakumbuka ilikuwa ni tarehe 14-12 siku ambayo Lady Jay Dee
kwa mara ya kwanza alipoandika kwenye mitandao ya kijamii ujumbe uliosema “ukinikosea
nitakusimamisha na sitokuamsha tena”,
Niliambiwa na jamaa wa Bongo5 na nikaamua kumpigia simu JD siku hiyo na nikamwambia kwamba,
kuna maneno nimeambiwa kwamba wewe umeandika, yeye akasema hapana, namini
nikamwambia sikiliza nikwambie kwa ninavyokwambia wewe , haya mambo hayafai.
Baada ya kukata simu dk 10 akanitumia sms mfululizo, ya kwanza
aliandika “Nililipa matangazo yangu ya laki 2 na 70, nimeambiwa kwamba umekataza
yasipigwe.
Sms nyingine ilisema “unaruhusu watangazaji wako wanitukane
na kui-promote bendi yako ya Skylite”.
Huku akiendelea Ruge akasema, unajua kwamba sisi biashara yetu
ni matangazo, kwa nini nikatae, mbona siku zote tunayarusha matangazo yao? Na Gadna
kila siku anakuwepo hapa kufanya matangazo? Ni swala la yeye kupita tu chini ni
kuuliza kama kweli matangazo hayarushwi.
Na kitu kingine ni kwamba, sio kweli na siwezi kumruhusu
mtangazaji yeyote amtukane redioni.
Mimi ishu ya skylite, Skylite wanalipa matangazo kama wateja
na bendi nyingine zinavyolipia, na huwa tunawapa bonsai kama ambavyo huwa
tunampa yeye JD.
Nilimwambia JD angalia maana ni kweli kwamba Skylite
wanakuja juu aangalie, hakika kuna upotoshwaji Skylite kuhusishwa Clouds,
Skylite ni ya Sebastian Ndege, yeye analipa matangazo kama wengine wanavyolipa,
akilipa laki 2 tunampa matangazo ya laki mbili kama bonasi.
Skylite ilichukua wanamuziki watatu wa Machozi Bendi, kama
ambavyo ilifanya kwa bendi Banana na TID.
Kiukweli wakati haya yanaendelea mimi nilikuwa safari
niliporudi baada ya hiyo tarehe 14,nikaona mbona hakuna jambo la kuzungumza au
kujadili, katika yote ni nini anacholalamika hasa? Mbona sioni tatizo?
Ishu ya kusema kwamba nyimbo zake hazipigwi, unajua hapa
kwetu kuna systeme ambayo inaweza kuangalia na kujua wimbo katika muda flani
ulichezwa mara ngapi, kupitia systeme hiyo tuliangalia na kuona kwamba wimbo
wake wa Joto Hasira ulichezwa mara 46 mpaka siku tunasema hatupigi nyimbo zake.
Tarehe 12-02 niliongea na Gadna na sio Jd juu ya kwenda kuazima
stuli kwa ajili ya shooting, na tukazitumia na kisha tulizirudisha.
Ni kweli kwamba tulikaa kikao binafsi sikuona kama kuna haja
ya kutopiga nyimbo za JD, baada ya kutuma sms ya kwamba sisi tunaogopa ndipo tukasema Redio ina policy kwa utaratibu wetu,
kwa anayetutukana, kutukebehi au maneno yoyot, basi nasi tutatumia njia zetu, na
mpaka mtu huyo aje kwetu na tuongee na ku-apologize.
Mbona Diamond nyimbo zake hazipigwi Magic fm mwezi wa saba
sasa, kuna kipindi Fulani East Afrika walikuwa hawazipigi nyimbo za Ray C na pia
za Alikiba.
Sikuwahi kuona kwa nini jambo hilo kufanywa la kitaifa.
Kuna Redio 82 hapa
nchini, na mtu anapokwambia achane kupiga nyimbo yangu, kwa maana asipotaka
yeye mwenye kwa kauli yake tusipige nyimbo yake, basi tunacha.
Ni utaratibu tu….
Sioni tatizo la wananchi kulifanya jambo hili kama la
kitaifa, kuna fulsa ya kujadili mambo mengi, kama ingekuwa mtu wa kugalagala
chini kwa kuchukuliwa wanamuziki basi angekuwa ni Asha Baraka, ila ila kila
siku kwa zaidi ya miaka 10 sasa anaamka anasimama, ndivyo ambavyo Lady Jay Dee
anapaswa kufanya.
Historia ya JD ni ndefu, kwa mara ya kwanza nilimsikiliza
kwenye Redio yetu kupitia kipindi cha Taji liundi cha Apex, alikwa studio
anarap, nikamwambia Taji nahitaji kesho aje ofisini, nilipoongea nae nikampa
kazi ya kutangaza, alikaa kwa kipindi cha mwaka mzima bila kuimba, mara ya
kwanza kumuweke ilikuwa ni kwenye wimbo wa Baba wa Taifa mwaka 99.
Nikasema huyu mtu ni msanii mzuri na aanze kuimba, tulirekodi
kwa Mika Mwamba na kwa msaada wa Mzee Muta.
Sisi tukanzisha project ya Smooth Vibe yenye lengo la
kuwajenga wasanii, kisha tukawambia mziki ni full time job na tuliwauliza je
mnachagua kuimba au utangazaji? Lady Jd na Ray C wakachagua kuimba na Fina
akaamua kuendelea na utangazaji.
Ilipofika miaka mitano na tulipoona project imekwenda vizu
tukaseama tuiache , tukaachana na project hiyo na yeye aaendelea zake.
Kinachotuhuzunisha ni kwamba yeye ni kioo cha wasanii
wachanga ambao wanatakiwa kuiga mfano wake kwa yale mazuri, na hapa ndipo penye
taizo ambalo ni kuachiana kijiti, tatizo ambalo ni kubwa kwa wanamuziki wengi
kujiandaa.
JD anatakiwa ajitahidi kutengeneza uwazi kwa watu wajaribu
kuelewa, sisi ni watu kama yeye, anashindwa basi atafute watu, na kama kuna
tatizo la kitaasisi, mimi nipo wazi tayari kukutanana naye na kutafuta muafaka juu
ya hili.
Mtu kama Lady Jay Dee anapaswa kufikisha malalamiko yake kwa
sehemu husika huku akiwa na vielelezo ili tuone muafaka wake.
Ni vyema kuwaandaa wasanii wetu na wao wajiandae, naamini
bado mda upo kwake yeye, cha msingi ni kwa yeye kurudi na kulisoma soko.
Swala la Clouds kwamba inataka kuuwa muziki wa bongo fleva
kwa makusudi, Clouds inategemea muziki wa bongo fleva kama mahudhui ya kipindi.
Clouds kila weekend ndio Redio peke yake inayotoa udhamini
kwa wasanii kufanya show zao Maisha na Bilicanas. Tamasha letu tunalofanya pekee
ni Fiesta ndani ya miezi miwili kwa mwaka, hii ina maana kwa miezi mingine 10
wasanii huwa wanafanya show zao zaidi yah ii ya kwetu.
Swala kwamba tulitaka kumpa laki nane akakataa, ni swalala
makubaliano, ni kama vile mbavyo unweza kumpa msanii million mbili akakataa au
mwengine ukampa laki sita akakubali, ni swala la makubaliano tu na ndivyo
biashara hii na nyingineyo kwa vile ilivyo
Ni kama yeye aliposhindwana Linah na Barnaba sababu ya
kiwango cha hela ambacho alitaka kuwapa.
Mimi nafikiri, JD inabidi akaze buti, anapigana wrong war, Skylite
inamsumbua na akubaliane na ukweli kwamba hilo ndilo tatizo lake.
Sielewi connection ya Nyumbani Lounge kwa Clouds na Ruge,
binafsi nintachojua vita zake azielekeze kwa Skylite Bend na inabidi azielekeze
huko, na aangalie tatizo lilitotokea Nyumbani Lounge naamini hiyo ndiyo sababu
kuu.
Cha msingi atafute mtu mwenye busara aangalie hili jambo
hili litaishaje.
Kwa kumalizia, hii nchi sasa na vyombo vinavyohusika inabidi virudi na kufanya
kazi zake ipasavyo kwa mambo mbalimbali yanayotokea kwenye mitandao.
Swala la kulaumiana halitatukuza, sisi ni Redio binafsi na
tutafanya kile tunachotakiwa kufanya kwa matakwa ya walio wengi, chochote
kinachotokea katikati.
Hii ni redio binafsi na sisi tuna taratibu zetu, kama
ambavyo tuliwa kupiga nyimbo za wanawake kwa siku nzima basi na kuanzia sasa
leo tusipige bongo fleva.
Msimamo wa kampuni, hili jambo hili hatutalizungumza, ila tunamtakia
kila la heri kwenye show yake ya tarehe 31, ila atakapokuwa tayari kuendelea kufanya biashara na saisi katika
zile redio 82 tutakuwa tayari kufanya kazi naye.
We are positive……
Safi sana kionghozi, nimekusoma @luge mutahaba the big bos
ReplyDeletesafi sana. japo najiuliza je mbona tuhuma hizi hazitofautiani sana na zile za kina sugu za wakati ule. anyway, umejibu poa mkuu
ReplyDeleteNi sawa ila mbona nyie mmekua gumzo sana na hii p funk inakuaje hebu funguka tena
ReplyDelete