Wednesday, May 08, 2013

Rappa Ja Rule Aachiwa Baada Ya Kifungo Cha Miaka Miwili

Baada ya kukaa jela kwa muda wa miaka miwili kwa kosa la kumiliki bunduki bila kibali na kukwepa kulipa kodi, msanii wa muziki wa hip hop toka nchibi Marekani, Ja Rule ameachiwa.

Ja Rule aliachiwa kutoka kwenye gereza kuu la Ray Brook ndani ya jiji la New York jana Jumanne May 6, ila ataendelea kutumikia kifungo akiwa nyumbani mpaka tarehe 28 July.

Ja Rule alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa makosa mawili, makosa ambayo aliyatumikia sambamba kwa jumla ya miezi 28.

No comments:

Post a Comment