Monday, May 20, 2013

Kauli Ya Sugu Iliyochafua Bunge Leo

Sugu
Bunge la Jamuhuri ya Muungano linaloendelea mjini Dodoma muda mfupi uliopita ilibidi liahirishwa na Spika wa Bunge, Bi. Anna Makinda.
 
Bi. Makinda amelazimika kusitisha shughuli za Bunge hilo mwanzoni tu mwa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliyokuwa ikiwakilishwa na Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu.

Kwenye hotuba hiyo iliyobabisha Spika wa Bunge asitishe shughuli za leo asubuhi hadi jioni Mh. Sugu ilisema, “Tanzania imegeuka chini ya usimamizi wa Wizara ya Serikali hii ya CCM kuwa Taifa linalotekanyara Wanahabari, kuwatesa, kuwangoa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali na hata kuwaua.”

Kufuatia kauli hiyo, Spika aliamua kusitisha Bunge ili kupata muda wa kuipitia hotuba hiyo na kuondoa kauli za uchochezi zitakazoonekana zipo ndani yake.

No comments:

Post a Comment