Msanii wa muziki wa kizazi kipya Chid Beenz, amesema watu wengi wanayafatilia maisha yake sababu yeye ni msanii mkubwa na ni star zaidi yao.
Chid ambaye masikani yake ni Ilala Flats jijini Dar, amesema kitendo cha watu kuwa wanamfatilia kwa yale au kile anachokifanya sababu yeye ni msanii mkubwa na wasanii wengine inabidi wamfuatilie.
Maoneno hayo yalikuja baada ya kumuuliza swali juu ya alichokisema Kala Pina, kwamba Chid ameathiriwa na madawa, ndipo Chid alipojibu, “Sasa yeye mwenyewe mbona anavuta ganja, vitu kibao anafanya, sasa kwani mbona mimi simtangazii kwenye media, mimi sina habari, yeye kama ananifatilia hivyo nashukuru kumbe mimi ni bonge la star.
Aliendelea Chid akisema, “Umeona Dan Chibo watu wanahisi nimepotea,
wakati kina Pina wananifatilia hadi maisha yangu, oohhh navuta nini…., sijui nimetoboa
nini….., nilihisi hajawahi kuniona na kaona nimefanya nini…., nimevaa niko nini……,
kumbe wananiona hivyo hadi nafanya nini, safi sana…” Alimalizia Chid Beenz…
No comments:
Post a Comment