Toka kwa Msomaji
Habari Wadau, binafsi nimekuwa kwenye mahusiano na msichana wangu kwa muda wa miaka mitano sasa.
Na ikafika kipindi nilimuomba tuoane na akakubali kuolewa na mimi. Baada ya kuafikiana juu ya siku na tarehe kwa ajili ya ndoa yetu ya kimila, eti wazazi wake wanataka nitoe mahari ya shilingi milioni tano.
Nilimueleza mpenzi wangu hiyo hela mimi sina na kumuomba aongee na wazazi wake japo wapunguze iwe milioni mbili, ila wazazi wake wamekataa.
Wanasema familia yao ni kubwa, wakiwa bado na wajomba na baadhi ya ndugu wengine.
Hakika sielewi nini cha kufanya, ila kiukweli nampenda msichana wangu na yeye ananipenda pia.
Nahitaji ushauri wenu.
Asanteni..!
No comments:
Post a Comment