Sunday, January 05, 2014

Nguli wa Mpira wa Miguu Eusebio Afariki Akiwa na Miaka 71

 
Mchezaji nguli toka nchini Ureno Eusebio, aliyetambulika kama mmoja kati ya washambuliaji bora waliowahi kutokea katika historia Duniani amefariki akiwa na umri wa miaka 71, vyombo vya habari nchini Ureno vimetaarifu mnamo siku ya Jumapili.
Jamaa huyu ambaye pia alitambulika katika kusimamia haki za mtu mweusi, ambaye jina lake kamili ni Esuebio da Silva Ferreira alizaliwa nchini Msumbiji ila alilifanya jina lake kutambulika na kuwa kubwa akiwa mshambuliaji wa Ureno kwenye fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1966 zilizofanyika nchini Uingereza, ambapo yeye ndiye alikuwa mfungaji bora wa michuano hiyo akifunga magoli tisa na kuiwezesha timu yake kushika nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo.

Alishinda taji la Ulaya akiwa na timu ya Benfica mnamo mwaka 1962 na kutajwa kuwa mchezaji bora wa Ulaya kwa mwaka 1965.

Gazeti la michezo la Ureno liitwalo A'Bola lilisema Eusebio amefariki mapema alfajiri ya Jumapili kutokana na shinikizo la damu.

No comments:

Post a Comment