Monday, April 29, 2013

Mtoto Wa Michael Jackson Akutana Na Mama Yake

Paris Jackson Na Mama Yake
Hii ni picha ya kwanza inayomuonyesha mtoto wa Michael Jackson aitwaye Paris Jackson, akiwa na mama yake aliyemzaa Debbie Rowe.
Wawili hao walikutana kwenye siku ambayo Paris alikuwa anasherehekea miaka 15 ya kuzaliwa kwakeya kuzaliwa, picha amabyo ilipigwa Ahi Sushi ndani ya Studio City, pande za Calif mnamo April 3, 2013.
Kwa mujibu wa Rowe, ambaye ni mke wa zamani wa Mfalme huyo wa muziki wa Pop, wawili hao walisherehekea kwa kufanya shopping na kuwa na muda mzuri wa mama na mwanawe.

Kwenye ukurasa wake wa twitter Paris ali-twee kwenye siku yake ya kuzaliwa: "Asante kila mmoja kwa pongezi zenu za siku hii!! ninyi ni watu wazuri na nawapenda!!"

Rowe, 54, alioana na Jackson mnamo November 14, 1996, jijini Sydney, Australia, na baadae kuja kuachana na nyota huyo wa muziki mnamo Oct. 1999.

Walibahatika kupata watoto wawili wakiwa pamoja: wa kwanza ni Prince Michael Jackson Jr., aliyezaliwa February 13, 1997, na Paris Jackson, aliyezaliwa April 3, 1998.

Watoto wote wawili wanaishi na mama wa Michael Jackson, aitwae Katherine Jackson, ambaye pia ndie muangalizi wa mtoto wa mwisho wa Michael aitwaye Prince Michael Jackson II, mwenye umri wa miaka 11.

No comments:

Post a Comment