Tuesday, April 30, 2013

Michael Jordan Aoa Kwa Mara Ya Pili

Michael Jordan na Mke Wake Yvette Prieto
Mchezaji nguli wa zamani wa NBA na mmiliki wa Charlotte Bobcats, Micheal Jordan ameoa kwa mara nyingine tena.

Hii ni mara baada ya pili kwa nyota huyo wa zamani wa mpira wa kikapu kuoa baada ya kuachana mke wake wa kwanza aliyeishi nae kwa miaka 17, kuzaa naye watoto watatu kisha kutengana mnamo mwaka 2006.

Micheal Jordan na mchumba wake, Yvette Prieto, mwenye miaka 35 ambaye ni modo, walichumbiana mnamo mwezi December na kuonana nae mwisho wa juma lililopita pande za Palm Beach, Florida, kwenye shughuli iliyohudhuliwa na ndugu pamoja na marafiki wachache.

Reception ya harusi hiyo ilifanyika kwenye kiwanja cha gofu cha Jordan, kilichopo karibu na nyumbani kwake. Huku wanamuziki kama Robin Thicke na mshindi wa Tuzo za Grammy Usher na The Source wakitumbuiza kwenye sherehe hiyo.

 
Hongera Michael Jordan na Mke Mpya....

No comments:

Post a Comment