Shetta Akiwa Amelazwa |
Msanii mkali wa muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilali maarufu
kama Shetta ni mgonjwa akiwa amelazwa kwenye Hospitalia ya Dr. Ameer jijini Dar,
kwa sasa msanii huyo amelazwa akiwa hoi akisumbuliwa na ungonjwa wa Maralia.
Shetta anayetamba na ngoma ya Sina Imani alinieleza,
hali yake ilikuwa mbaya sana ila kwa sasa ana nafuu japo bado bado amelazwa katika
hospitali hiyo iliyopo maeneo ya Kariakoo jijini huku akiwa maetudikwa dripu.
alipoongea na mimi kwa njia ya simu Shetta alisema, tangu wiki iliyopita alikuwa anajisikia vibaya, hali yake ilibadilika gafla na kuwa mbaya zaidi siku moja mara baada ya kutoka kufanya
show kwenye moja kati ya kumbi za jijini Dar.
“Hali ilikuwa sio nzuri, ila namshukuru Mungu kwa maana sijawahi
kujisikia vibaya kama ambavyo nimejisikia pindi nilipoletwa hapa, ila kwa sasa
najisikia nafuu zaidi mara baada ya kupata matibabu, nililetwa hapa siku ya
Jumamosi na sikuwa kwenye hali nzuri hata kidogo” alisema Shetta.
Wakati anafanyiwa vipimo Shetta alionekana kuwa na Maralia
tano, ndipo ilipobidi aanzae dozi huku
akitundikiwa dripu mfululizo za maji.
Akiongea kwa sauti ya chini Shetta alinieleza “hivi
niniavyoongea na wewe ndio nimepata hata nguvu ya kupokea simu, maana nilikuwa
nipo nje ya mawasiliano kwa siku mbili sasa, na hii ni kutokana na hali mbaya
niliyokuwa nayo, namshukuru Mungu kwa maana naendelea vizuri, na hali
ikiendelea kuwa hivi naweza kuruhusiwa kutoka” alisema Sheta.
Ugua Pole Shetta…..,
No comments:
Post a Comment