Tuesday, April 30, 2013

Mchezaji Wa NBA Afichua Kwamba Yeye Sio Ridhiki

Jason Collins
Mchezaji wa kati kwenye ligi ya mpira wa kikapu ya nchini Marekani (NBA) Jason Collins amekuwa mwanaume wa kwanza anayecheza kwenye michezo mikubwa ya kulipwa kukiri kwamba si ridhiki.

Jamaa mwenye umri wa miaka 34, ambaye amewahi kuichezea timu za Washington Wizards na Boston Celtics katika msimu uliopita, aliwaeleza waandishi wa habari za michezo:

"Sikupanga mimi ndio niwe mtu wa kwanza ambaye nacheza kwenye timu kubwa ya Marekani kusema nipo hivi. Ila sababu kweli niko hivyo, najisikia raha kuanzisha mazungumzo haya. Natamani nisingekuwa kama mtoto nipo ndani ya darasa kisha akinyoosha mkono na kusema 'nipo tofauti'. Kama ningekuwa na njia zangu, basi kuna mtu mwengine angekuwa ameshafanya hivyo. Hakuna aliyefanya hivyo, na ndio sababu nainua mkono wangu juu.

Collins aliendelea, "Wakati nipo mdogo nilikutana na mwanamke. Na pia nilimchumbia. Nilidhani nilihitajika kuishi maisha hayo. Nilidhani nahitaji kumuoa mwanamke na kulea watoto nae. Nimekuwa nikijiambia mwenyewe kwamba anga ingekuwa nyekundu, ila nilifahamu mara zote kwamba ni ya blue."

No comments:

Post a Comment