Kutana na mtoto millionea mwenye umri wa miaka sita aitwae Isabella,
ambae aliupata utajiri huo mara baada ya kushinda shindano la urembo.
Isabella alifanikiwa kushinda thamani za watoto kwenye shindano la urembo, fedha ambazo
zimemfanya kuingiza dola million moja za kimarekani mnamo mwaka 2012.
Mama yake Suzanna Barrett alisema kwamba Isabella anajua
fasheni na huwa anapenda kujaribu kila aina ya bidhaa zinazowekwa sokoni. Huwa anachagua
aina mpya za mikufu na kuijaribu kuzivaa zikiwa kwenye rangi tofauti na
kuziweka kwenye kabati lake.
Isabella Akiwa Ofisini |
Licha ya kwamba mama yake ndie hufanya maamuzi ya kibiashara, lakini Isabella ndie kichwa nyuma ya mambo yote.
Akizungumzia maisha yake ya ki-superstar, Bella alisema , “Ni nani asiyependa kuwa millionea? Mimi ni superstar, nina lebo yangu ya thamani mbalimbali na napenda kuwa bosi. Sijawahi kupoteza chochote, maana kila shindano ninaliongia huwa nashinda. Ila ninachopenda zaidi kuliko vyote ni viatu, kwa maana nina zaidi ya pea 60.”
Je, Jamii yetu inatoa fursa kwa kuendeleza vipaji halisi vya watoto wetu...?
Isabella Na Thamani Zake |
No comments:
Post a Comment