Kim na Kanye |
Kanye amekuwa akisafiri kwenye miji kadhaa kwa miezi sasa kwa ajili matukio, kuimba na kurekodi album mpya, ila hayp hayamzuii kuwepo kila ambapo Kim atahitajika kwenda kumuona daktari.
Tumeelezwa kwamba Kanye huwa anafanya safari japo tatu kwa kutumia ndege binafsi kutoka Paris kwenda L.A safari ambazo huwa zinatumia hela nyingi.
Chanzo hicho pia kimesema kwamba, Kanye amefikia hatua ya kwenda kuonana na dokta kwa ajili ya kupanga ahadi mapema, ili aweze kupanga mambo yake ili aweze kuwepo pale Kim atakapohitajika kwa daktari.
Kwa mujibu wa chanzo, Kanye amemsafirisha Kim kwenda Paris kwa ndege binafsi ili aweze kuwa nae kwenye muda wa ziada kabla ya Kim hajajifungua mnamo mwezi wa saba.
No comments:
Post a Comment