Prosper Dzakpasu |
Jamaa mmoja aitwae Prosper Dzakpasu wa kijiji cha Dzodze
Ablorme kilichopo Ketu, Kusini mwa Volta nchini Ghana, ameripotiwa kuishi kinyumba
na dada yake wa damu kwa miaka 12 sasa.
Licha ya tahadhali na vitisho vya watu mbalimbali, Prosper, 38, amegoma kuacha kulala pamoja na dada yake.
Vyanzo karibu na familia vilielezea gazeti la DAILY GUIDE kwamba, baada ya kugundua hali hiyo walimkanya, ila kutokana na kukaidi kwake ndipo ilipowapelekea kuijulisha jamii juu ya swala hili.
Waligundua juu ya huo mwenendo, hata Mama wa watoto hao naye
alikuwa na shaka juu mwenendo wao, kwa mara kadhaa aliwataka waachane na tabia hiyo. Ila licha ya jitihada
zake Mama mzazi wa watoto hao alichoka na kuamua kukaa kimya.
Prosper ni mtoto wa kwanza miongoni mwa watoto watano kwenye familia, wakati Cynthia ni mtoto wa mwisho kuzaliwa.
Babu yake na Prosper, ambaye pia aligundua hali hiyo, mara kadhaa na kwa wakati wake alijaribu kuwakanya lakini ilishindikana.
Watoto wengine watatu
nao hawakuwa wamependezwa na mwenendo huo na hawakuwa na namna yoyote kuweza
kuzuia mahusiano hayo yasiendelee.
Inasemekena Prosper
alianza kutembea na dada yake, Cynthia Dzakpasu, ambaye kwa sasa ana umri wa
miaka 29 kipindi ambacho alikuwa na miaka 17.
Mahusiano hayo ambayo
yalianza taratibu, yalikuwa sio siri, kwani kipindi hicho walikuwa wanaishi
kama mke na mume, wakiwa wanaishi pamoja sehemu moja iitwayo Dzodze Ablorme,
huku Prosper akiwa anjishughulisha na kazi za kushona nguo.
Baada ya kuonywa mara kadhaa na watu kwenye familia yao ambao
mwanzoni walikuwa wanaificha hali hiyo, Prosper peke yake akaamua kupotea
pasipojulikana kwa miaka mitano.
Baadae ikaja julikana
kwamba alikimbilia Accra kwenda kufanya kazi, baada ya wiki chache, alikuja
kumchukua dada yake na kwenda kuishi kwenye nyumba ambayo haikufahamika jijini
Accra.
Hakuna ambacho
kilifahamika mpaka mwaka mmoja uliopita walipoamua kurudi Dzodze wakiwa na mtoto
wa kike mweye miaka sita.
Chanzo hicho kiliieleza DAILY GUIDE kwamba “Prosper kwa sasa amezidi kuwa kiburi na anaonekana kutomuheshimu au kumuogopa tena mtu yoyote. Kwa maana anajua mtu yeyote atakapo kutana nae au kumuita itakuwa anataka kuongea juu ya uchafu wake, kwa hiyo hatokuja na hata akija hatomjali mtu yoyote kwa lolote atakalolisema.”
Chanzo hicho kiliieleza DAILY GUIDE kwamba “Prosper kwa sasa amezidi kuwa kiburi na anaonekana kutomuheshimu au kumuogopa tena mtu yoyote. Kwa maana anajua mtu yeyote atakapo kutana nae au kumuita itakuwa anataka kuongea juu ya uchafu wake, kwa hiyo hatokuja na hata akija hatomjali mtu yoyote kwa lolote atakalolisema.”
Chanzo hicho kimeeleza,
familia imeamua kulifikisha suala hilo Polisi ili Prosper akamatwe na
kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa wa sheria za nchi.
Baadhi ya ndugu,
ambao walishindwa kuelewa kwanini ndugu hawa wameamua kujiingiza kwenye
mahusiano haya ya ajabu, wamehusisha kitendo hiki ni masuala ya nguvu za giza,
wakati wengine wamehusisha kitendo hicho na laana.
No comments:
Post a Comment