Aliyekuwa Boyfriend wa mwanamziki wa hit single ya Hips Don’t Lie aitwae Shakira,
amefungua kesi ya madai dhidi ya mrembo huyo ambae kwa sasa anatokana mkali wa
mpira wa miguu anayekipiga kwenye klabu ya Barcelorna ya Hispania aitwae Geralrd
Pique.
Jamaa amefungua kesi ambayo anahitaji kulipwa kiasi cha Dola za Kimarekani 250 Millioni, huku dai lake kuu ni juu ya yeye kuhusika kwa kiasi kikubwa kwenye mafanikio ya mkali huyo wa Waka Waka.
Antonio de la Rua ameanzisha tifu la kimataifa dhidi ya ex wake, akisema
kwamba yeye ndie ambaye amefanikisha kukuza “nembo ya Shakira”, huku
akisisitiza kuwa alihusika kwenye mafanikio ya ngoma zake mbili ambazo zimemuweka
juu mdada huyo, akizitaja ngoma za Hips Don’t Lie” na “Waka Waka” kuwa kuna
mkono na akili zake zilihusika katika kufanikisha mafanikio ya ngoma hizo.
No comments:
Post a Comment