Wednesday, February 26, 2014

Joel Campbell Mchezaji wa Mkopo wa Olympiakos Toka Arsenal Aiua Machester United [PICHA]

Manchester United inahitaji kushida kwa zaidi ya goli 2-0 kwenye mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Olympiakos mara baada ya kupokea kipigo cha idadi hiyo ya magoli kwenye ardhi ya Ugiriki.

Mashetani hao wekundu walijikuta wakifungwa goli la kwanza zikiwa zimebaki dakika saba kabla ya mapumziko mara baada ya Alejandro Dominguez kwa bahati kuugusa mpira uliopigwa na Giannis Maniatis uliogonga mguu wa kipa David de Gea na kuzama nyavuni.

Mambo yalizidi kuwa mabaya kwa vijana wa David Moyes mapema kwenye kipindi cha pili, pale Joel Campbell - mchezaji wa mkopo wa Olympiakos kutoka Arsenal - alipokimbia na mpira kisha kupiga shuti la mguu wa kushoto toka umbali wa yadi 30 na kuingia wavuni kwenye kona ya chini kuandika bao la pili.










No comments:

Post a Comment