Fatma Binti Baraka maarufu kama Bibi Kidude amefariki dunia leo.
Chanzo cha kifo chake ni maradhi ya kiuskari, kwa mujibu wa mmoja kati ya wajukuu zake aitwae Omari alinieleza kwamba Bi Kidude amefariki leo mida ya saa saba na nusu mchana.
Akiendelea kuongea Omari alisema "takribani miezi mitano iliyopita, marehemu alikuwa anasumbuliwa na kisukari, kilichomsababishia kupata uvimbe mwilini mwake."
Aliongeza kwa kusema, kwa kipindi chote hicho walijaribu kumpeleka hospitali ila hali yake haukutengemaa mpaka umauti wake ulipomkuta leo hii.
Taarifa za awali zinasema msiba upo Raha Leo, Unguja, na mazishi yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Kitumba
Fatuma binti Baraka au Bi Kidude, alizaliwa katika kijiji cha Mfagimarigo Zanzibar katika familia ya watoto saba (7). Baba yake Mzee Baraka alikuwa ni mfanyabiashara wa nazi, zao ambalo ni la kutumainiwa sana Zanzibar. Bi Kidude anasema hafahamu tarehe halisi aliyozaliwa, isipokuwa anachojua ni kwamba alizaliwa wakati rupia ikitumika kama fedha, na vilevile ana hakika ni kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Ulaya. Wataalamu wa mahesabu baada ya kupata taarifa hizo wakampigia mahesabu na kumkabidhi miaka yake kwamba ni zaidi ya miaka 90.
Bi Kidude ni msanii mkongwe na mahiri sana katika fani ya muziki wa mwambao ambao hujulikana kwa jina la Taarabu. Muziki huu ambao ni mchanganyiko wa muziki toka nchi za Kiarabu na vionjo vya muziki wa Kiafrika umekita sana katika mwambao wa Afrika Mashariki yaani Zanzibar, Mombasa, Lamu na kwingineko.
Bi Kidude anasema uimbaji aliuanza tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi na alijifunza kutoka kwa msanii mkongwe na aliyetamba sana enzi hizo Sitti binti Saad. Anasema wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakifika Zanzibar kuja kumwona Sitti, na kwa vile Bi Kidude na Sitti walikuwa wako karibu basi yeye alikuwa akiwapeleka wageni wale nyumbani kwa Bi Sitti, wakifika huko wageni walikuwa wakiingia ndani na yeye kubakia nje, kule ndani Bi Sitti alikuwa akiwaimbia wale wageni, na yeye huku nje alikuwa akimsikiliza kwa makini na kumfuatiza jinsi alivyokuwa akiimba. Aliendelea hivyo hadi akawa mahiri sana katika uimbaji.
Chanzo cha kifo chake ni maradhi ya kiuskari, kwa mujibu wa mmoja kati ya wajukuu zake aitwae Omari alinieleza kwamba Bi Kidude amefariki leo mida ya saa saba na nusu mchana.
Akiendelea kuongea Omari alisema "takribani miezi mitano iliyopita, marehemu alikuwa anasumbuliwa na kisukari, kilichomsababishia kupata uvimbe mwilini mwake."
Aliongeza kwa kusema, kwa kipindi chote hicho walijaribu kumpeleka hospitali ila hali yake haukutengemaa mpaka umauti wake ulipomkuta leo hii.
Taarifa za awali zinasema msiba upo Raha Leo, Unguja, na mazishi yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Kitumba
Bi Kidude Enzi Zake Akiwa Studio |
Bi Kidude ni msanii mkongwe na mahiri sana katika fani ya muziki wa mwambao ambao hujulikana kwa jina la Taarabu. Muziki huu ambao ni mchanganyiko wa muziki toka nchi za Kiarabu na vionjo vya muziki wa Kiafrika umekita sana katika mwambao wa Afrika Mashariki yaani Zanzibar, Mombasa, Lamu na kwingineko.
Bi Kidude anasema uimbaji aliuanza tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi na alijifunza kutoka kwa msanii mkongwe na aliyetamba sana enzi hizo Sitti binti Saad. Anasema wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakifika Zanzibar kuja kumwona Sitti, na kwa vile Bi Kidude na Sitti walikuwa wako karibu basi yeye alikuwa akiwapeleka wageni wale nyumbani kwa Bi Sitti, wakifika huko wageni walikuwa wakiingia ndani na yeye kubakia nje, kule ndani Bi Sitti alikuwa akiwaimbia wale wageni, na yeye huku nje alikuwa akimsikiliza kwa makini na kumfuatiza jinsi alivyokuwa akiimba. Aliendelea hivyo hadi akawa mahiri sana katika uimbaji.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Bibi Kidude Mahala Pema Peponi.
No comments:
Post a Comment