Suma G |
Msanii mkongwe kwenye gemu la muziki wa kizazi kipya kutoka kwenye kundi la Hot Pot Family, Suma G anatarajia kuachia video yake mpya hivi karibuni ndani ya mwezi huu itayokwenda kwa jina ‘Wima’ , akipewa sapoti ya kutosha na msanii kutoka kundi la Wanaume Family, Chege Chigunda a.k.a fundi chuma.
Ngoma imefanyika chini ya Makaveli Records na Producer Muba Tachi.
Msanii huyo alietamba na nyimbo nyingi kama vile ‘Vituko uswahilini’, ’Watu hawakai’, pamoja na ‘Destination’.
Msanii huyo alietamba na nyimbo nyingi kama vile ‘Vituko uswahilini’, ’Watu hawakai’, pamoja na ‘Destination’.
Akiongea na nami, Suma G alisema ”kwasasa ninaamua kutoa video kabla ya audio kwa kuwa watu wengi wamenisahau kwenye mziki huu hivyo video zangu zitawakumbusha, kwaiyo naomba mashabiki wangu pamoja na Hot Pot Family kwa ujumla kukaa tayari kupokea video mpya pamoja na kazi zangu nyingi.”
No comments:
Post a Comment