Monday, September 01, 2014

Polisi Ujerumani Wamuokoa Diamond Kutoka kwa Mashabiki Wenye Hasira [PICHA]

Ukumbi uliharibiwa na washabiki mjini Stuttgart, Ujerumani
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30, Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri, mwanamuziki nyota wa mziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, Ujerumani, mara baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show yake.

Imeelezwa kwamba mashabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi za kiasi cha Euro 25 kwa kiingilio ambapo walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 usiku ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.

Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki  Diamond na promota wake. Inaelezwa kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki.

Ma-Dj walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa,  mmoja wa Djs hao alipoteza Laptop yake huku Dj wa kike aliyejulikana kama Flor alipatwa mshtuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo  Dj Drazee ambaye naye yupo hoi hospatal mpaka sasa.


Polisi nchini ujerumani wanamesema tukio hilo ni la aibu sana sababu halijawahi kutokea, kwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani watu wa nchi hiyo hueshimu sana suala la muda wao.

Mpaka sasa polisi wanamsaka muandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashtaka promoter huyo ambaye ni raia wa Nigeria, huku pia ikiongezwa kwamba Polisi pia inamchunguza zaidi kwa kusemekana anajihusisha na mtandao flani wa biashara haramu.

Baadhi ya magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wa hasira nawe DIAMOND"  cheki link hii: http://www.stuttgarter-nachrichten.de/inhalt.blaulicht-aus-der-region-stuttgart-31-august-diamond-platnumz-zieht-aerger-der-fans-auf-sich.ca1f4b9d-599b-4c95-84c8-fe25d10b6ed9.html

No comments:

Post a Comment