Thursday, August 28, 2014

Kikosi cha Timu ya Manchester United Ndicho Chenye Gharama Zaidi Kwenye Premier League kwa Sasa

Ghali: Kiasi cha £60m za Angel Di Maria kuja Manchester United toka Real Madrid imefanya jumla ya pesa za kusajili kikosi cha United kuwa zaidi ya £400m 
Kusajiliwa kwa Angel Di Maria wiki hii kumefanya jumla ya pesa zilizotumika kwa ajili ya kusajili wachezaji wa kikosi hicho kufika £401.2m - huku ikiaminika kiasi hicho cha pesa kinaweza kuongezeaka kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Thamani ya kikosi cha United sasa imepiku ile ya majerani zao na mabingwa watetezi Manchester City, ambao kikosi chake thamani yake ni£344.15m kwa ujumla.

Hizi ni timu tano na thamani ya vikosi vyao... 

1. Manchester United £401.2m
2. Manchester City £344.15m
3. Chelsea £341.8m
4. Liverpool £245.8m
5. Arsenal £209.5m

No comments:

Post a Comment