Thursday, May 29, 2014

Malcolm Glazer Aliyekuwa Mmiliki wa Manchester United Afariki Dunia

Aliyewahi kuwa mmiliki wa klabu ya Manchester United, Malcolm Glazer, amefariki dunia mnamo siku ya Jumatano akiwa na umri wa miaka 85.

Glazer, aliyeinunua  United mwaka 2005, pia anamiliki timu ya kwenye ligi ya NFL iiitwayo Tampa Bay Buccaneers, ambao ndio waliotangaza habari ya kifo chake kwenye mtandao wao.

Tajiri huyo ambaye ni mfanyabishara toka Palm Beach, Florida, amekuwa na matatizo ya kiafya toka mwezi April 2006 pale alipopata ugonjwa wa kiharusi uliomfanya ashindwe kuwa anaongeana vizuri na pia uliomfanya apooze mkono na mguu wake wa kulia.

Chini ya umiliki wa Glazer, United walifanikiwa kushinda mara tanoPremier Leagueve times, pia na kutwaa Champions League mwaka 2008.

"Mawazo ya kila mmoja ndani ya Manchester United yapo pamoja na familia yake usiku huu," klabu hiyo ya kwenye Premier League ilisema.

No comments:

Post a Comment