Wednesday, April 09, 2014

HABARI YA KUSIKITISHA: Nguli wa Mchezo wa Mieleka wa WWE, Ultimate Warrior Afariki Dunia

Siku chache baada kutoka kwenye WWE Hall of Fame na miaka 18 kurudi kwenye shirikisho hilo, nguli wa mchezo wa mieleka, The Ultimate Warrior amefariki Dunia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa WWE, nyota huyo wa mchezo wa mieleka amefariki akiwa na miaka 54.

Habari hizio ziliwekwa kwenye mtandao huo mnamo siku ya Jumanne usiku, zilizopelekea kutumwa kwa salamu nyingi za rambirambi toka kwa washabiki wa WWE na viongozi mbalimbali.

Kwenye taarifa yake, shirikisho hilo lilisema, "WWE imeshtushwa na inasikitika kupokea habari za kifo cha nguli na nyota wa WWE, The Ultimate Warrior.

No comments:

Post a Comment