Thursday, March 13, 2014

Rais wa Bayern Munich Jela Miaka Mitatu na Nusu kwa Kukwepa Kodi

Rais wa timu ya Bayern Munich Uli Hoeness amekutwa na hatia ya kosa la kukwepa kulipa kodi na Mahakama ya nchini Ujerumani siku ya Alhamisi na kuhukumiwa kwenda jela kwa miaka mitatu na nusu.

Wakili wa Hoeness baadae alitangaza kwamba wana mpango wa kukata rufaa kwenye Mahakama Kuu ya haki nchini Ujerumani.


Jamaa huyo mwenye umri wa mika 62 alihukumiwa kutokana na kutolipa euro 3.5 million ($4.85 million) kwenye kodi za hela zilizokuwa kwenye akaunti benki ya nchini Uswizi.

No comments:

Post a Comment