Tuesday, December 10, 2013

Michael Jordan Kuitwa Baba kwa Mara Nyingine Tena


Nguli wa timu ya Chicago Bulls, Michael Jordan, anategemea kuitwa baba kwa mara nyingine tena. Mke wake ambaye ni modo mwenye mchanganyiko wa ki-cuba na ki-marekani, Yvette Prieto, anategemea kujifungua mtoto wao wa kwanza, jarida la watu maarufu, US Weekly limeeleza mnamo siku ya Jumamosi.

Bado muda ambao mtoto huyo atazaliwa haijajulikana.

Jordan, 50, na Prieto, 34, walioana mnamo mwezi April ndani ya Florida baada ya miaka mitano ya mahusiano yao. wawili hao wanaishi karibu na Miami.

Mpaka sasa Jordan ana watoto watatu ambao aliwapata kwenye ndoa yake ya awali ambayo alidumu nayo kwa miaka 17 na mwanamke aitwaye Juanita Venoy, iliyovunjika mnamo mwaka 2006.

No comments:

Post a Comment