Monday, December 09, 2013

Drogba na Eboue Kupigwa Faini na Chama cha Soka cha Uturuki kwa Kuandika Ujumbe wa Maandishi wa Kifo cha Mandela


Didier Drogba na Emmanuel Eboue watatozwa faini na chama cha mpira cha Uturuki baada ya kuonyesha vesti ambazo zilionyesha ujumbe wa kuguswa kwao na kifo cha Nelson Mandela.

Wachezaji hao wawili wa kimataifa toka Ivory Coast waliziweka wazi hisia zao kwa ujumbe huo mara baada ya mechi ya Galatasaray dhidi ya Elazigspor mnamo siku ya Ijumaa, kwenye mechi ya kwanza toka kifo cha kiongozi huyo wa Afrika Kusini kilipotokea.



Nguli huyo wa Chelsea, Drogba alivua jezi yake kwenye mechi iliyoisha kwa kushinda 2-0 na kisha kuonyesha kuguswa kwake na kifo hicho, ambapo maandishi kwenye vesti yake yalisoma: ‘Thank you Madiba’ huku yale ya nyota wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Eboue yalisema: ‘Rest in Peace Nelson Mandela’.




No comments:

Post a Comment