Monday, December 23, 2013

Baada ya Kichapo Toka kwa Mahasimu Wao Yanga Yamtimua Kazi Kocha Wake Brandts



Muda mchache uliopita klabu ya Yanga imetangaza kumtimua kocha wake Raia wa Uholanzi aitwaye Ernie Brandts, hii ikiwa ni siku chache tu baada ya kufungwa mabao 3-1 na mahasimu wao Simba kwenye mchezo wa maalum ya Mtani Jembe.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, mkataba wa Brandts umesitishwa rasmi leo hii asubuhi na ameshakabidhiwa barua ya kumtaarifu juu ya hali hilo.


“Tumesitisha mkataba na kocha wetu na ameshakabidhiwa barua yake, huo ni uamuzi wa uongozi mzima wa Yanga, kila kitu kimeenda sawa katika kuachana naye,” alisema Kizuguto.

Hivi karibuni Yanga walimuongeza mkataba kocha huyona wameamua kuuvunja kwa kutoridhishwa na kiwango kinachooneshwa na timu hiyo licha ya kufanya usajili wa nguvu wa kikosi chake.

Brandts anaondoka kwenye klabu hiyo huku akiwa amewapa ubingwa wa ligi kuu msimu uliopita na akiiacha timu hiyo ikiongoza ligi mpaka mzunguko wa kwanza unamalizika.

Kocha msaidizi Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Razak Siwa wao wanaendelea kubakia katika timu hiyo.

Itakumbukwa Brandts alitua Yanga akitokea APR ya Rwanda msimu mmoja nyuma.


CHANZO: Vyanzo Mbalimbali

No comments:

Post a Comment