Marehemu Dj Rankim Ramadhani |
Akizungumza nami mda si mrefu mtu wa karibu na marehemu aitwaye Mabruki Rwehumbiza alisema, Marehemu amefariki kutoka na kusumbuliwa na tumbo kwa muda mrefu.
"Mara baada ya kufanyiwa uchunguzi Marehemu alibainika kuwa na matatizo kwenye njia ya utumbo, na mara baada ya kugundulika hivyo alitakiwa kufanyiwa oparesheni."
Aliendelea kwa kuongeza "mapema leo hii Marehemu alipelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kufanyiwa oparesheni, na kwa bahati mbaya alifariki wakati akiwa kwenye hatua ya kufanyiwa oparesheni." alisema Rwehumbiza.
Mipango ya mazishi bado haijafahamika, ila nitazidi kukupa taarifa zaidi kadiri nitakavyokuwa nazipata.....
Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Rankim Ramadhani Mahala Pema Peponi...
No comments:
Post a Comment