Friday, May 10, 2013

Ronaldo Aweza Kurudi Old Traford Huku Rooney Akiwa Na Mpango Wa Kubaki


David Moyes na Wayne Rooney wakizungumza

Kuna taarifa zinazoendelea kwamba, winga wa timu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo anaweza kurudi Old Trafford.
 
Gazeti la Daily Mail limetanabaisha kwamba Mtendaji Mkuu wa kalbu hiyo David Gill, amekuwa ndani ya jiji la Madrid kukutana na Jorge Mendes, ambaye ni ajenti wa Ronaldo, huku lengo ni katika kupatana juu ya uwezekano wa mchezaji huyo kurudi Man U kwa dili moja ala ukweli.
Daily Mail na magazeti mengine yametaarifu pia kwamba klabu ya Bayern Munich ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa timu ya Manchester United Wayne Rooney,ambaye inaaminika kwamba amewaeleza wachezaji na meneja wake kwamba ataruhusu ofa toka Ujerumani.

Kwa mujibu wa BBC , Wayne Rooney ambaye anathaminishwa kwa dola 30 millioni anaweza kubaki kwenye timu hiyo ya Manchester United, kutokana na kuteuliwa kwa Meneja wa Everton David Moyes.

No comments:

Post a Comment