Friday, May 10, 2013

Rick Ross Amvisha Pete Mchumba Wake Yenye Thamani Ya Dola Laki Tano



Rozay Na Shateria
Hili nimeligundua wikiendi iliyopita, msanii katika miondoko ya hip hop toka nchini Marekani Rick Ross, amemvisha petet ya uchumba aliyekuwa demu wake wa siku nyingi Shateria.
Shateria ambaye ni mtu wa mitindo na mambo yote yanayohusu wanawake wazuri, ila kitu cha msingi ni kwamba demu huyu ni aina ya mwanamke ambaye ana uwezo wa kumtuliza mtu.

Shateria alikuwa na Rick Ross toka kipindi ambacho alikuwa ni rapa mdogo, na muda wote amekuwa yupo na Rozay, hata mapema mwaka huu ambapo rapa huyo alitaka kuuwawa pia siku hiyo walikuwa pamoja (walikuwa pamoja kwenye gari naye).
Rick anafahamu upendo wa dhati alionao Shateria, na katika kile kinachoonekana kuthamini hilo tunataarifiwa kwamba rapa huyo ameamua kumvisha pete ya madini ya almasi, ambayo ina thamani ya dola za kimarekani 500,000.

 Hongera kwa Rozey na Shateria….!

No comments:

Post a Comment