Sunday, May 05, 2013

Mourinho Ataka Terry Na Lampard Wabaki Chelsea

Terry Na Lampard
Tetesi mpya kutoka Stamford Bridge zinaeleza kwamba, Jose Mourinho atafurahi zaidi kama wachezaji wawili wa timu ya Chelsea, John Terry na Franck Lampard, watabaki kwenye klabu hiyo, kama zoezi la yeye kurudi timu hiyo litafanikiwa kwenye msimu ujao.
 
Kwa mujibu wa gazeti la Sun la nchini Uingereza, Jose Mourinho atahitaji wachezaji wote wawili Lampard na Terry wamsaidie kubeba kombe la Ligi Kuu ya nchi hiyo, kombe ambalo kwa mara ya mwisho walilibeba kwenye msimu wa 2009/10 wkiwa chini ya kocha Carlo Ancelotti.

No comments:

Post a Comment