Tuesday, May 21, 2013

Majanga Kwa Mary J. Blige, Anadaiwa Dolla Milioni 3.4 Kwa Kukwepa Kodi

Mary J. Blige
Licha ya kutokea kwa skendo za ukwepaji wa kodi zinazowakabili watu wengi maarufu kwa wiki iliyopita, mamlaka inayoshughulikia Mapato ya nchini Marekani (I.R.S.) bado inaendelea na zoezi hilo.

Habari moto kwa sasa ni hii inayomuhusu ya Malikia wa Hip-Hop Soul, Mary J. Blige, kwa mujibu wa TMZ inasemekana kwamba, Blige anatuhumiwa kwa kutolipa kodi zake zote za mwaka 2009, 2010, na 2011.

I.R.S. imesema kwamba mwimbaji huyo wa wimbo wa “I’m Goin’ Down” anadaiwa kiasi cha dolla za Kimarekani zipatazo 3,426,255.43.

No comments:

Post a Comment