Kwanza kabisa, kwenye maelezo yangu nakuomba usionyeshe jina langu. Binafsi huwa naipenda sana blog yako, na kiukweli nimekuwa nikiifatilia sana.
Mimi ni Mtanzania ila kwa sasa naishi kwenye nchi moja iliyopo Barani Asia nikiwa nasoma.
Ipo hivi, nimekuwa kwenye mahusiano na boyfriend wangu kwa zaidi
ya mwaka sasa, mtu ambaye naye yupo huku nilipo.
Wiki chache zilizopita amebadilisha status yake ya mahusiano
kwenye Facebook, na kwa sasa inaonyesha yupo kwenye mahusiano na mwanamke
mwengine na sio mimi.
Nilijisikia vibaya sana , nilipomuuliza aliniambia hakuna
lolote linaloendelea kati yake na mwanamke huyo na cha msingi anasema nimuamini....
Ila hataki kuitoa hiyo status, anasema ataitoa muda mwingine
sio kwa sasa. Kwa muda wa wiki sasa tumekuwa tukizungumza na kiukweli nampenda
sana, sijui cha kufanya.
Tafadhali naomba ushauri, nachanganyikiwa....
Asante.
No comments:
Post a Comment