Friday, May 24, 2013

Album Ya KATO By Wakuvanga (Orijino KomediI) Kuzinduliwa Mwishoni Mwa Mwezi Huu

Album Kava
Wakuvwanga Entertainment wanatarajia kuanzisha kampeni ya kwanza kwa kampuni hii ambayo inahusisha usambazwaji wa DVD za album ya kwanza ya Wakuvwanga inayojulikana kama KATO.
 
Kwenye taarifa iliyosambazwa na msemaji wa kampuni hiyo Mwasu Mpore, imeeleza kwamba album hii inatarajiwa kuzinduliwa na kuanza kuuzwa tarehe 31 May 2013 siku ya ijumaa kuanzia saa 12 asubuhi.
 
Tuna hakika kwamba wewe ni mmoja kwenye timu ya wapigania haki za wasanii na una uwezo wa kuitangaza na kuilinda kazi hii kwa hali na mali.

Jumla ya pikipiki 5 zinategemea kutolewa wakati wa uuzaji, pikipiki ambazo zitapatikana kwa mtu yeyote ambaye atapata bahati ya kununua DVD yenye label ya pikipiki ndani.
 
Tutakuwa na magari matano ambayo yatazunguka mji wa Dar Es Salaam kwa siku zote tatu maalum kwa wananchi watakaonunua rejareja kwa siki za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.
 
Katika kufanyia promosheni album hii mpaka sasa zimeshatoka video mbili toka kwenye album hiyo Angwisa na Vatu, huku audio zake nazo zikiwa zimetoka na kufanya vizuri.
 
Kwenye picha hapo juu tumeunganisha muonekano wa kava ya DVD hii na audio za tracks zilizokwisha kwenda hewani kwa uonekano mzuri.
 
Wanunuzi wa jumla watatakiwa kupiga simu zifuatazo ili wapate maelekezo ya wapi wanapoweza kuupata mzigo watakaotaka na kuupata.

0656-621807 Famy
0718-852828 Waku
0717-792023 Mwasu

No comments:

Post a Comment