Friday, April 19, 2013

Nick Minaj na Pink Wireless Pill Speaker

Nick Minaj, rapa wa kike ambaye kwa sasa dunia inatambua uwepo wake, anaudhihirishia ulimwengu kwamba anamaanisha kuwa yeye yupo kibiashara zaidi na kutumia kila njia itakayowezekana  kuingiza hela mfukoni mwake, kumaanisha huku kunatokana na kuamua kwake kuanzisha cha kumuingizia hela nje na muziki.

Rapa huyo anategemea kuwa mshindani mkubwa wa headphone maarufu za“Beats by Dre” baada kuanzisha spika za pinki zisizotumia waya (pink wireless pill speaker). Rapa huyo hana haraka, ametulia taratibu kimtindo akifanya yake, huku lengo lake kuu ni kuhakikisha anaingiza kila hela inayowezekana kwa kupitia muziki na biashara mbalimbali. Hivi karibuni alisaini dili kubwa na “American Idol,” na huyu hapa tena na uwekezaji mwengine.

No comments:

Post a Comment