Saturday, April 20, 2013

Kweli Mungu ni Mkuu


Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 32, siku moja akiwa anavuta sigara huku anaendesha gari, alivuta pafu moja kisha akapulizia moshi wa juu na kusema “Mungu hii ni kwa ajili yako”.
Naye akiwa na umri wa miaka 32 alikufa kwa maradhi ya Kansa.

Jamaa aliyetengeneza meli ya Titanic
Baada ya kuitengeneza meli hiyo, muandishi mmoja alimuuliza, je meli hii itakuwa na usalama kiasi gani?
Kwa kejeli alimjibu: ‘Fahamu hata Mungu haweza kuizamisha'
Matokeo yake: Naamini wote mnafahamu nini kilitokea kwa meli ya Titanic

Marilyn Monroe (Aliyeigiza muvi hiyo)
Siku moja alialikwa na Billy Graham kwenye kipindi kimoja .
Marilyn akamwambia, roho ya Mungu imenituma kwako nikupe neno.
Baada ya kusikia ambacho Muhubiri alimwambia, yeye akajibu:
'Simuhitaji Yesu wako'.
Wiki moja baadae, alikutwa amekutwa amefariki kwenye nyumba yake

Bon Scott (Mwanamuziki)
Muimbaji wa zamani wa kundi la AC/DC. Kwenye wimbo wake alioutoa mwaka 1979 aliimba hivi:
“Usinizuie, natembea zangu njia nzima mpaka kwenye barabara ya motonil'.
Tarehe 19 February 1980, Bon Scott alikutwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha.

Ilitokea Campinas (mwaka 2005)
Ndani ya Campinas , Brazil, kundi la marafiki wakiwa wamelewa, walienda kumchukua rafiki yao wa kike nyumbani kwao.....
Mama wa rafiki huyo alimsindikiza kwenye gari na alikuwa na hofu sana kwa vile ambavyo rafiki zake walikuwa wamelewa, akamwambia mtoto wake huku akiwa amemshika mkono na wakati tayari akiwa ameshakaa kwenye gari:
'Mwanangu, na utembee na Mungu kwa maana atakulinda.'
Yule msichana akajibu: Kama yeye (Mungu) na aweza basin a atembee kwenye magari makubwa kwa maana hili letu dogo limeshajaa'
 Masaa machache baadae taarifa ilifika, kwamba kwenyehiyo  safari kumetokea ajali, na wote waliokuwa ndani ya lile gari wamefariki, na gari lao halikutambulika lilikuwa ni la aina gani.

Watu wengi wanajisahau kwamba hakuna jina lingine kuu zaidi ya jina la Mungu.

Mimi nimefanikisha upande wangu kwa kukushirikisha wewe kwenye hili, basi nawe ni jukumu lako kuhakikisha unalifikisha hili kwa wengine unaowali.

Ni rahisi sana, fanya tu kuwaeleza watembelee blog hii ili wapate ujumbe huu: http://danchibo.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment