Hii inashangaza….. kwa sababu kwenye mahojiano yake
aliyoyafanya na Toolz kwenye Tv ya Ndani, D'banj alisema kwamba yeye ni mtu mwenye furaha kwa sababu
anatoka na mwanamke ambaye yupo nae kwa muda sasa.
Jana wakati anafanyiwa mahojiano na Seun Apara wa Thisday,
D'banj alisema kwamba yeye yupo singo na hajampata mwanamke sahihi mpaka sasa.
D'banj alimueleza Seun:
"Nimekuwa kwenye mahusiano na wanawake wengi ila
nisingependa kuongea kuhusu wao, sababu wengi kati yao wameenda na mambo yao au
wameolewa. Sina ninachijutia kabisa sababu mimi bado ni kijana na sijaoa, japo
mama yangu anataka nitulie. Mama yangu ananipenda na binafsi namfanya aelewe
kwamba sio kama sitaki kuoa, ila bado sijampata mwanamke sahihi. Kama ataweza
kunitafutia mwanamke sahihi , anaweza kuniita.
No comments:
Post a Comment