Sunday, June 08, 2014

Mzee Small Afariki Dunia

Muigizaji mkongwe nchini Said Ngamba maarufu kama Mzee Small amefariki dunia siku ya Jumamosi majira ya saa 4 usiku akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar.

Mzee Small aliyejizolea umaarufu kutokana na uigizaji wake mahili amefariki kwa ugonjwa wa kiharusi mara baada ya kuugua kwa muda mrefu kabla ya kuzidiwa na kupelekwa Muhimbili.

Mtoto wa marehemu aitwaye Muhidin amethibitisha kifo cha Baba yake. 

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMINA...!

No comments:

Post a Comment