Wednesday, June 04, 2014

Je ni Kweli Kwamba Beyonce Ana Mahusiano ya Siri na Mlinzi Wake [PICHA]

Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, inasemekana kwamba Jay Z anapatwa sana na wivu kutokana na ukaribu wa Beyonce na mlinzi wake aitwaye Julius (mtalaka mwenye mtoto mmoja), akidhani kuwa wawili hao wana mahusiano.

Huyu ndiye yule yule mlinzi aliyejaribu kumlinda Jay Z dhidi ya shambilizi la kwenye lifti. Jamaa yupo karibu sana na Beyonce, mara zote mikono yake huwa ipo karibu ya mwanamuziki huyo.

Inaeleweka ni kwa nini Jay Z anakuwa hajisikii poa, ukweli ni kwamba jamaa anamfahamu sana Jigga, amekuwa naye kwa kipindi kirefu sasa toka mwaka 2009, na ndiye mtu pekee ambaye anaufahamu ukweli wa ile habari ya ugomvi uliotokea kwenye lifti.

Inaelezwa kwamba siku hiyo mlinzi huyo alionekana kumlinda Beyonce kwa kiasi kwamba, mara baada ya ugomvi huo, Jay Z alitaka yeye na Beyonce waingie kwenye gari la Solange ila mlinzi huyo alimuongoza aingie kwenye gari lingine.

Cheki picha zao hapo chini kisha nipe majibu...










No comments:

Post a Comment