Monday, June 09, 2014

Filippo Inzaghi Achukua Nafasi ya Clarence Seedorf Kuifundisha AC Milan

Klabu ya AC Milan amemfukuza kazi kocha wake Clarence Seedorf baada ya kipindi kisichozidi miezi mitano toka ashike nafasi hiyo, huku ikimtaja Filippo Inzaghi kama mrithi wake.

Mchezaji huyo wa zamani wa Italia Inzaghi, 40, amesaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu hiyo huku akiachana na kazi ya kufundisha timu ya vijana ya timu hiyo.


Seedorf, 38, alichukua nafasi hiyo toka kwa Massimiliano Allegri mwezi January akiiacha timu hiyo ikimaliza ligi ya Seria A kwenye nafasi ya 11.

No comments:

Post a Comment