Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola ametania kuwa huwa anapata wakati mgumu zaidi kufafanua juu ya mbinu yake ya kubadili wachezaji kwa mke wake Cristina kuliko anavyopata shida hiyo kumueleza mchezaji kama Arjen Robben.
Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona mara kadhaa amekuwa akiwapumzisha wachezaji wake wenye uwezo mkubwa akiwemo Mholanzi huyo kutokana na ukubwa wa kikosi cha timu aliyonayo.
Mke wa Guardiola anaamini kwamba mume wake angekuwa bora zaidi kama angekuwa anachezesha wachezaji walioshinda kwenye mechi ya awali, Goal imetaarifu.
“Mke wangu Cristina mara kadhaa amekuwa akilaumu juu ya mbinu zangu,” mchezaji huyo wa zamani kimataifa wa Hispania aliwaeleza waandishi. “Amekuwa akiniambia natakiwa kupanga kikosi kilichoshinda mechi ya mwisho.
“Kumueleza juu ya mtindo wangu wa kubadili wachezaji ni mgumu zaidi ya kumwambia Arjen Robben kuwa benchi la mechi inayofata linamuhusu… -
No comments:
Post a Comment