Gazeti moja nchini Ubeligiji mnamo siku ya Jumatatu imebidi liombe radhi kutokana na kitendo chake cha kutoa picha ya Rais wa Marekani Barack Obama akiwa na First Lady Michelle Obama picha ambayo imefanyiwa photoshopped iliyowaonyesha wakiwa wamefanana na sokwe. Sambamba nayo picha hiyo iliyochapishwa pia kulikuwa na nyingine iliyoeleza kuwa Obama ni muuza bangi.
Picha hizo zilitokea kwenye makala maalum ya gazeti la De Morgen ambayo ilitoka kwenye toleo lake la Jumamosi. Kwenye picha hiyo gazeti hilo pia lilitania kwamba Rais wa Russian Vladimir Putin ndiye aliyeituma picha hiyo.
Mkanganyo huo umekuja huku Rais huyo wa Marekani akitegemea kufanya ziara nchini Ubeligiji siku ya Jumanne.
No comments:
Post a Comment