Friday, February 14, 2014

NAOMBA MSAADA: Ameniacha Ghafla Leo Hii! Nasherehekea Vipi Valentine Nikiwa Peke Yangu..?

Nimekuwa kwenye mahusiano na mtu wangu kwa miaka miwili sasa. Jana tu, alianza kubadilika nikahisi ni utani. Aliniahidi kunitoa kwa ajili ya Valentine ili aweze kunipa furaha za kimapenzi na hata tulifanya mapenzi jana hiyo hiyo.

Leo ikiwa ni siku ya Valentine sijui kwa nini ameamua kuanzisha ugomvi na mimi. Nasikia wanaume wengi wanafanya hivyo sana, ila sikuwahi kufikiria kama mtu wangu anaweza kunifanyiia hivyo. Nimemuomba sana msamaha ila hataki kunisikiliza….

Kiukweli sijafanya kitu chochote kibaya. Kwa nini wanaume wanakuwa kama mambwa. Nahuzunika jamani, naomba ushauri nifanyeje....?

No comments:

Post a Comment