St Valentine ni mtu wa upendo; alionyesha upendo kwa yeyote aliyetokea mbele yake kuanzia wagonjwa, walemavu, watoto wasio na wazazi, wafungwa, masikini na hata matajiri. Sababu kubwa ya kwa nini anakumbukwa kila inapofika tarehe 14 Februari ilikuwa ni kwa sababu na kujitoa kwake kwa ajili ya rafiki yake wa toka udogoni....
St Valentine alikuwa ni mchungaji ambaye alijitolea kufa kwa niaba ya rafiki yake ambaye alituhumiwa kwa makosa, yeye (St Valentine) aliona kwamba rafiki yake wa toka udogoni hakuwa na makosa, tarehe 14 Februari ilipangwa kuwa siku ya kunyongwa kwa huyo rafiki yake ila St Valentine alikuwa na wazo lake binafsi na akasema;
‘’KAMA RAFIKI YANGU ATAKUFA, MKE NA WATOTO WAKE WATAKUWA WAKILIA MARA ZOTE KWA KUMKUMBUKA YEYE, ILA YEYE (ST VALENTINE) ALIONA AKIFA YEYE HAKUTAKUWA NA MKE AU WATOTO WATAKAOLIA KWA SABABU YAKE.”
Hivyo akaamua kuyatoa maisha yake kwa ajili ya rafiki yake na hiyo ilikuwa ni tarehe 14 Februari.
NDUGU ZANGU NA JAMAA, Siku ya Valentine ni yakuonyesha upendo wa kweli na sio haya mapenzi ya kidunia, hebu na tuitumia katika kuuenzi upendo wa kweli aliokuwa nao ST VALENTINE.
No comments:
Post a Comment