Kwa mujibu wa taarifa, Curtis Jackson anategemea kuanzisha maisha mapya akiwa na G-Unit Records kama lebo inayojitegemea.
50 Cent anaondoka Interscope, lebo ambayo ilimtoa kwenye ulimwengu wa muziki na mafanikio, anaondoka na lebo yake ya G-Unit Records na kwenda kufanya kazi kivyao.
Rapa huyo aliyezaliwa Queens, amesaini makubaliano ya usambazwaji wa kazi zake Duniani kote na Caroline/Capitol/UMG, ikiashiria uwezekano wa kutoka kwa album yake mpya ya Animal Ambition mnamo June 3.
Dili hiyo ilitangazwa kupitia vyombo vya habari kutoka kwenye lebo hiyo, huku ukiondoa mwisho wa kipindi ambacho 50 Cent amekuwa kimya kwa kutotoa album toka alivyofanya hivyo mnamo mwaka 2009 alipotoa album yake ya mwisho ya studio iliyojulikana kama Before I Self Destruct.
Kiongozi wa Shady Records, Eminem naye ameshatoa kauli kutokana na kuondoka gafla kwa 50 Cent huku akisema, "Wote kwa binafsi yangu na Shady Records kwa ujumla tunashukuru kupata nafasi ya kuwa pamoja na 50 kitaaluma," alisema kwenye taarifa yake.
"Shady kwa ufupi haitokuwa kama ilivyo bila ya 50 Cent. Nilianzisha urafiki mkubwa na 50 kwa miaka kadhaa, na hiyo haitobadilika. Tunajua 50 atakuwa na mafanikio kwenye mipango yake mipya, na tutaendelea kumuunga mkono yeye na G-Unit." (Forbes imeandika)
No comments:
Post a Comment