Wednesday, December 11, 2013

Ribery Atajwa Kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka Ufaransa


Mshambuliaji wa Bayern Munich, Franck Ribery, ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka nchini Ufaransa na Jarida la Mpira wa Miguu la Ufaransa.

Ribery mwenye umri wa miaka 30 amewapiku viungo wawili Paul Pogba wa Juventus na wa Paris St Germain, Blaise Matuidi, kwenye kura zilizopigwa na wachezaji wa zamani na wa sasa wa Ufaransa.

Franck Ribery ni mmoja kati ya wachezaji watatu wanaogombea tuzo ya 2013 ya FIFA Ballon d’Or.

Ribery, amefanikiwa kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bundesliga na Kombe la Ujerumani akiwa na Bayern mwaka huu, pia ametajwa kwenye idadi ya watu watatu kwa ajili ya Tuzo ya FIFA-Ballon d’Or mnamo siku ya Jumatatu sambamba na mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.

Kocha wa AS Roma, Rudi Garcia, ambaye amejiunga na timu hiyo ya Serie A akitokea Lille ambaye mpaka sasa hajafungwa kwenye mechi 15 za ligi, alitajwa kuwa Kocha bora Mfaransa kwa mwaka 2013 kwenye kura zilizopigwa na mameneja wa zamani na wa sasa.

Ribery mpaka sasa ameshinda taji hilo mara tatu, mara mbili nyuma ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal FC, Thierry Henry.

No comments:

Post a Comment