Waziri wa zamani wa Wizara ya Mambo Nje wa Marekani Hillary Rodham Clinton, amesema bado hajaamua kama atagombea Urais kwa mwaka 2016 ila “atafanya maamuzi hapo mwakani”.
Akiongea kwenye mahojiano kwenye televisheni, Clinton alisema kwamba ni “uamuzi mgumu” na hataki kuharakisha juu ya hilo.
Alisema kwenye mahojiano hayo kwamba kitu cha kuangalia inatakiwa ni ukosefu wa ajira, watu kutolewa kwenye biashara ndogondogo ambazo haziingiza faida.
Kwa sasa Clinton ndiye anayeonekana kuongoza kama muwakilishi wa chama cha Democratic atakaye mrithi Rais Barack Obama.
Mwanamke huyo ambaye ni first lady wa zamani kwa sasa anaandika kitabu kinachohusu maisha yake ya Idara ya Ikulu ambacho kitatoka mwakani.
No comments:
Post a Comment