Marehemu Erasto Msuya |
Mazishi ya kifahari yanaandaliwa na familia ya marehemu Erasto
Msuya, huku ikielezwa kuwa jeneza litakalotumika kubeba mwili wake
linafunguka kwa kutumia ‘rimoti’
Msuya aliyeuawa wiki iliyopita, anazikwa leo huku
familia ikitangaza kutokulipiza kisasi kwa waliohusika, badala yake
wamemwachia Mungu.
Kinachovutia katika msiba huo ni jeneza lililobeba
mwili wa mfanyabiashara huyo lililoagizwa Nairobi, la aina yake huku
likifunguliwa kwa kutumia ‘rimoti’.
Jeneza hilo lililoagizwa kutoka Kampuni ya
Montezuma & Monalisa Funeral Home, linafunguliwa kwa kubonyeza kifaa
maalumu hata mhusika anapokuwa mbali.
Hali hiyo ilionekana kuwaacha na mshangao maelfu
ya waombolezaji waliofika kuaga mwili wakati wa ibada iliyofanyika
nyumbani kwake, Kwa Iddi, wilayani Arumeru.
Mfanyabiashara huyo aliyeuawa kwa kumiminiwa
risasi zaidi ya 20 na watu wasiojulikana, anazikwa leo nyumbani kwao
eneo la Kairo Mirerani, Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.
Kaka wa marehemu, Israel Msuya, alisema jana kuwa
mazishi hayo yatafanyika makaburi ya familia ya mzee Elisaria Msuya
‘Kikaango’, baba wa marehemu Erasto.
Kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi ya mazishi hayo
inayoongozwa na kaka mkubwa wa familia ya Msuya, Gady, zaidi ya Sh100
milioni zimepangwa kugharimia shughuli za maombolezo na mazishi.
CHANZO: Gazeti Mwananchi
"zaidi ya Sh100
milioni zimepangwa
kugharimia shughuli za maombolezo na mazishi"
Imesema
Kamati ya Mazishi
CHANZO: Gazeti Mwananchi
No comments:
Post a Comment