Wednesday, April 24, 2013

Waziri Nchini Misri Ahukumiwa Miaka 25 Jela

Yousef Boutros-Ghali
Aliyewahi kuwa waziri wa Fedha nchini Misri amehukumiwa kwenda jela miaka 25 na Mahakama ya nchi hiyo, mara baada ya kukutwa na hatia ya kutumia vibaya mali za Umma.

Kwa mujibu gazeti la Serikali la Misri, kwenye taarifa yake iliyochapishwa siku ya Jumanne limeandika, Yousef Boutros-Ghali amekutwa na hatia ya kufuja mali za Umma zenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 3.6 kwenye mwaka wa mwisho wa uwaziri wake.

Boutros-Ghali ambaye ni mpwa wa Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Boutros Boutros-Ghali, hakuwepo mahakamani wakati hukumu yake inatolewa, huku ikiaminika kwamba alikuwa London nchini Uingereza.

Kutokuwepo kwake inamaanisha kwamba ana uwezo wa kukata rufaa punde atakaporudi toka huko.

No comments:

Post a Comment