Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha kilichopo eneo la Njiro nje kidogo ya jiji hilo, leo hii wamesambaratishwa na mabomu ya machozi ya kikosi cha kutuliza ghasia (FFU).
Hii inafuatia kitendo chao cha kumfanyia fujo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mlongo wakati alipoenda kuongea nao kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao aliyeuawa usiku wa kuamkia leo kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulikana.
Wanafunzi ambao idadi yao bado haijajulikana baadhi yao wanashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na kuhusika kwao katika fujo hizo.
No comments:
Post a Comment