Wednesday, April 24, 2013

Jengo Laanguka India Na Kuuwa Watu 80

Jengo Lililo Anguka
Watu wapatao 80 wamekufa na wengine wengi wanahofiwa kunaswa baada ya jingo la ghorofa 8 kuanguka katika mji mkuu wa Bangladeshi ,Dhaka , maafisa wa serikali nchini humo wameeleza..
Jitihada za kuwaokoa watu walionaswa chini ya kifusi cha jengo hilo zinaendelea na inaelezwa kwamba watu wapatao 200 wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Jengo hilo lipo katika eneo liitwalo Savar, na vikosi vya jeshi vimejiunga katika operesheni ya kuokoa watu walionaswa.
Kuanguka kwa majengo sio jambo geni nchini Bangladesh ambapo majengo mengi marefu hujengwa kinyume cha taratibu.
Jengo hilo la gorofa 8 lilikua na kiwanda cha nguo, benki pamoja na maduka. Lilianguka wakati wa pilikapilika za asubuhi.
Mamia ya watu wamekusanyika katika eneo hilo wakiwatafuta ndugu, jamaa na marafiki zao.
Taarifa zinaeleza bado haijajulikana chanzo cha kudondoka kwa jengo hilo, lakini vyombo vya habari nchini humo vinaeleza kuna nyufa ilionekana kwenye jengo hilo jana.

No comments:

Post a Comment