Tuesday, April 16, 2013

WAIGIZAJI HUFANYIKA NGONO WAKIWA LOKESHENI

Waigizaji wa movie nchini Nigeria wamekuwa wakijihusisha na matendo ya ngono pindi wanapokuwa lokeshen, mwanadada muigizaji Mojisola Olaiya maarufu kama Moji Olaiya amefunguka. Chini ni mahojiano kati ya mtangazaji mmoja wa Nigeria aitwae Kayode Aponmade na muigizaji huyo wa kike; Kayode Aponmade aliuliza: Je unakubali kwamba waigizaji huwa mna tabia ya kufanya mapenzi mnapokuwa lokeshen? Moji Olaiya akajibu: "Inawezekana, kufanya mapenzi ni mchezo wa kiutu uzima ambao unahitaji makubaliano ya watu wawili. Ikiwa hakuna hata mmoja aliyewahi kutoka na kusema amebakwa, basi hakuna haja ya kuwa na mjadala juu ya hilo." Kisha akamaliza kwa kusema "hata watu wengine kwenye fani zao hufanya mapenzi, si lazima wawe wameoana, waache waichukulie poa oooh" Je hali hii pia ipo kwa Waigizaji wa filamu za hapa kwetu ama..?

No comments:

Post a Comment